ENGINEERS REGISTRATION BOARD TANZANIA


ISO 9001:2015 Certified

News

MAFUNDI SANIFU WAFANYA UTALII WA NDANI HIFADHI YA TAIFA MIKUMI

May 9th, 2026

Baadhi ya Mafundi sanifu walioshiriki katika mkutano wa nane (AETD 2026) wakiwa katika hifadhi ya taifa ya Mikumi wakifanya utalii wa ndani .

Safari hiyo imeandaliwa na bodi ya usajili wa wahandisi (ERB) ikiwa ni sehemu ya kutangaza shughuli za kihandisi kupitia treni ya Kisasa ya SGR pamoja na kuhamasisha utalii wa ndani.

Baadhi ya washiriki wamesema hatua hiyo ni muhimu kwa wao kujumuika kwa pamoja na kujenga marafiki wapya katika taaluma yao ambapo pia wamesema utalii huo unawapa pumziko baada ya kuwajibika katika miradi mbalimbali.